Wakopwaji/wadaiwa wamekuwa
wakipata shida sana kutoka kwa wanaokopesha.
Mkopesha awe ni mtu binafsi,
taasisi ya fedha , kampuni binafsi au
mwingine yeyote wamekuwa wakiwasumbua sana wadeni
wao.
Kubwa zaidi hasa taasisi za
fedha hutumia masharti ya mikataba ambayo
huwa yameandaliwa kitaalam kiasi cha
mtu ambaye si mwanasheria kutoelewa kwa undani maana yake
kuwabana wadeni ambao hushtukia
masharti hayo baada ya kuwa wameshaanza kudaiwa.
Mbaya zaidi wamekuwa
wakifanya hivi bila kufuata taratibu za
kisheria. Kwakuwa wamemsaidia mtu kwa
kumkopa basi wamekuwa
wakiichukulia hali hiyo kama
leseni ya kufanya lolote ilimradi tu
wanadeni na wewe.
Mali za watu
huuzwa hovyo , wengine hufikishwa mpaka
vituo vya polisi ilimradi
tu wakopeshaji hupenda kupindisha
utaratibu. Hapa tutaeleza baadhi ya mambo
kadhaa ya msingi ambayo
mkopeshaji haruhusiwi
kumfanyia mdeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...