NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mh.Gaudensia Kabaka(watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau(wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama(wapili kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka(picha na Freddy Maro)
Jengo zuri hili jamani, kama sio Tanzania vile. Mungu bariki maendeleo nchini mwetu vita na malumbano yanarudisha nyuma maendeleo. Mungu ibariki Tanzania yetu.
ReplyDeletePongezi nyingi sana kwa NSSF chini ya Uongozi wa DC.Dau . Mmeendelea kuwa Mfano wa Kuigwa kwa Shirika la Umma linaloongoza kwenye kuleta Maendeleo ya wazi kwa WaTanzania Nchi Nzima. Juhudi zenu katika kuinua sekta Mbalimbali zinaonekana wazi. Hongera sana NSSF.
ReplyDeleteMdau Diaspora