Baada ya kugundua kuwa ujenzi wa nyumba hii iliyopo Bomang'ombe mkoani Kilimanjaro umeingia kwenye kiwanja chake ,mmiliki wa eneo hilo aliamua kujenga ukuta kuzunguka kiwanja chake na alivyofika katika nyumba hii alipitisha ukuta wake mlangoni.


Ukuta ukapita sebuleni mwa nyumba hiyo na kutokea nyuma ya nyumba.Na Hii ndio waswahili wanasema dawa ya Kiburi Jeuri.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hawa akina Masawe wana mambo.

    ReplyDelete
  2. Mie nadhani ni KIBURI moja kwa moja, kwa sababu hata kama huyo mwenye kiwanja chake kashindwa ku compromise na huyo mwenye banda lake hapo, basi vyombo vya sheria vingeingilia kati na kuchukuwa hatuwa husika kuutatuwa mgogoro huo wa kiwanja, kuliko kumkomowa mithli hiyo, waswahili wanasema...kiburi si maungwana. Na huyo alopitisha ukuta hapo kama kweli kafanya kwa kumkomowa mwenziwe tu ili ajifakharishe, basi hata fakhari tunaambiwa ni mama wa ujinga. Ama kweli hiyo ni zaidi ya kiburi au tuseme ni kiburi 'extra' maana hata huyo Abunuwasi hakufanya hivyo alikuwa na hekma zake na busara na suluhu ilipatikana kwa salama kabisa!

    ReplyDelete
  3. Half the world problems can be solved by talking. Kama hawa jamaa wangekaa na wasuluhi wangeweza kutatua ugomvi wao.Nyundo na msumari hawana mawasiliano ila ya kugongana.

    ReplyDelete
  4. HK inawezekana huyo mwenye kiwanja ameshachoka na danadana za "mgogoro tutautakuwa kesho". Lakini huo ukuta " halali" mbona kama umechoka,wa siku nyiiiiingi kuliko hilo banda lililoingia ktk uwanja wa mwenyewe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...