Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam imezuia maandamano ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya
Ilala (UVCCM) ya kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho pamoja na
kuacha kiporo maandamano ya Baraza la
Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).
Akizungumza leo na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ,Kamishina wa
Jeshi la Polisi ,Suleiman Kova ,amesema kuzuia kwa maandamano hayo inatokana na
kuwepo kwa taarifa za Kiintelejensia za kuvuruga amani.
Kova amesema maandamano ya UVCCM Wilaya ya
Ilala yalitakiwa kufanyika kesho lakini kutokana na kuwepo kwa taarifa za
kiintelejensia za Machinga ,Bodaboda ,Mama Lishe na Baba Lishe kushiriki
maandamano na kufikisha malalamiko yao
kupitia maandamano hayo.
Amesema kumekuwepo kwa taarifa katika
mitandao ya jamii wakihamasishana bodaboda na machinga ,mama lishe na baba lishe
kushiriki maandamano pamoja na kutoa ujumbe wao kwa kupitia maandamano katika
Mkoa wa Dar es Salaam .
Kova amesema machinga ,Mama lishe,Baba,na
Bodaboda watumie taratibu zingine za
kufikisha ujumbe kutokana na sheria zilizowekwa na sio kutumia mgongo katika
vyama vya siasa.
Kwa upande
Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA)
maandamano yao yalikuwa yanahusu kwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi ni lini
itaanza kuandikisha daftari la wapiga kura ,pamoja na wanafunzi watashiriki
vipi upigaji kura ambapo Kamanda Kova amesema hilo wanaweka kiporo kwanza
wanafanya uchunguzi wa taarifa mbalimbali.
“Sisi tunachoangalia amani kwani maandamano
ya amani yanaweza kufanyika lakini mwisho wa siku inakuwa sio amani kwa jeshi
la polisi tunawajibu kuangalia hilo ”amesema
Kamanda Kova.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...