Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika Machi 1, 2015 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro zimepata msisimko mpya baada ya wanariadha nyota wa Tanzania kuthibitisha kushiriki.
Mkurugenzi wa Mbio hizo John Bayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliwataja baadhi ya wanariadha nyota kutoka Tanzania kuwa ni Andrew Sambu, Daudi Joseph, Mashaka Masumbuko, watachuana na wanariadha wengine kutoka nchini na kutoka nje ya nchi katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanaume za kilometa 42.195.
Kwenye upande wa marathon wanawake Fabiolla William, Sarah Maja and Banuelia Katesigwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania watakaochuana na wenzao kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwania tuzo mbalimbali kwenye Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanawake za Kilometa 42.195.
Aidha, wanariadha Fabian Fabian Joseph, Alphonce Felix, Dickson Marwa wamethibitisha kushiriki Tigo Kili Half Marathon wanaume wakati Mary Naali, Natalia Elisante, Catherine Lange na Jacqueline Sakilu ni miongoni mwa majina maarufu katika riadha yaliyothibitisha kushiriki kupitia kundi la wanawake litakalochuana katika Mbio za Tigo Kili Half Marathon.
Katika mbio za nusu marathon ambazo Tanzania ina historia ya kufanya vizuri, Fabian Joseph ana rekodi ya ushinda Kilimajaro Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza mbio katika muda wa 1:3;59 na vilevile ana rekodi ya kushinda Edmonton Marathon mwaka 2005 kwa muda wa 1:01:08.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...