Wala hakosei kusema ‘kujua kazi ni raha’. Isha
Mashauzi anakushuka tena kivingine na wimbo mpya kabisa “Nimpe Nani” unaodhihirisha
kuwa anaijua vema kazi yake.
Hii ni ‘single’ yake ya pili nje ya taarab
ukiacha ule wa kwanza “Nimlaumu Nani” uliopigwa katika miondoko ya rhumba.
“Nimpe Nani” ni wimbo unaoelea kwenye miondoko
ya zouk rhumba lakini ukikolezwa kwa mbali na vionjo vya mduara.
Wimbo huo wa dakika tatu na nusu ambao umerekodiwa
katika studio za C9 Records chini ya producer C9 Kanjenje.
Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto na C9,
magitaa ya bass na solo yamepigwa na Babu Bomba wa Malaika Band.
Sauti zote tamu unazozisikia humo ni za Isha
Mashauzi kasoro sehemu ndogo sana isiyozidi sekunde 5 iliyotikiwa na Easy Man.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...