Na Chalila Kibuda
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene amesema kushuka kwa bei ya mafuta kuendane na hali halisi ya vitu vyote vinavyotumia nishati hiyo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na wadau wa mafuta kupata mawazo katika uendeshaji wa sekta hiyo,Simbachawene amesema kuwa kushuka kwa mafuta hata nauli ya kusafiri kwa daladala pamoja na mabasi ya mikoani na nje ya nchi ni lazima zishuke.
Simbachawene amesema watanzania wanataka kuona kushuka kwa mafuta kunaleta unafuu wa maisha na sio yanashuka katika soko lakini huduma zake zinabaki kama zilivyo,hata wale ambao wanasaga nafaka kwa kutumia nishati ya mafuta wanashusha bei zao kutokana na soko la mafuta kushuka na wananchi kuwa na imani mamlaka zinazoendesha soko hilo.
“Imani yangu ni kuona watanzania wanapata mafuta bora na bei inashuka kwa pande zote na sio kushusha upande mmoja huku upande mwingine unapata huduma iliyo juu”amesema Simbachawene.
Amesema wataendelea kufatilia uchakachuaji wa mafuta pamoja na umwagaji wa mafuta ili kuwe na uchumi imara na serikali kuendelea kupata mapato yake katika sekta hiyo,pia ataendelea kufatilia changamoto za wafanyabiashara wa mafuta ikiwemo suala la kodi kuwa kubwa.
“Kazi yangu ni kuangalia mafuta yanaendelea kuwepo katika nchi kwani bila mafuta hakuwezi kuwepo uchumi imara”amesema Simbachawene.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa mafuta ili kupata mawazo yao katika uendeshaji wa sekta hiyo,leo kwenye ukumbi wa JB Belmonte,jijini Dar es salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Charles Mwijage.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MOIL,Mansoor Shanif akichangia mada katika mkutano huo.
Sehemu ya wadau wa mafuta wakiwa kwenye mkutano huo.
TUMEZOEA MAFUTA YAKIPANDA BEI NDANI YA SIKU TATU UTASIKIA NAULI ZA MABASI ZINAPANDA DALADALA WANAPANDISHA BAJAJI NK SASA BEI IMESHUKA KIMYA.
ReplyDeleteKama ni hivyo, tutakupenda sana Mheshimiwa Simbachawene. Kazana na kuwa na uchungu na nchi yako na wananchi wako maskini.
ReplyDeleteJana,EWURA walijikanyaga katika kujibu swali ni kwa nini bei ya bidhaa kama umeme,nauli,n.k.havishuki?Kwa kweli kinara wa EWURA asituletee 'rongorongo' kwenye nyakati hizi za makompyuta yakokotayo takwimu ndani tu ya sekunde.
ReplyDelete