Na Bashir Yakub.
Hapa kwetu Tanzania habari ya kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara nyingi matendo haya yamekuwa yakifanywa na watu wenye uwezo kifedha dhidi ya wasio na fedha pia kati ya maofisa wa polisi na raia. Mtu kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua kumfungulia yeyote mashtaka. Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri tena. Siseme walio mahabusu, hao nao hawana idadi. Inasikitisha mno. Ni wazi kuwa wengi wao wamefikia huko aidha kwa kusingiziwa kosa na askari au mtu mwenye cheo au fedha. Lakini zaidi wametoka mikononi mwa askari kwakuwa hata huyo mwenye cheo au fedha hawezi kumbambikizia mtu kesi bila kupitia kwa askari. Kwahiyo askari ndio tatizo kubwa katika hili.
1.NINI MAANA YA KUBAMBIKIZWA KESI.
Kubambikizwa kesi au kumshtaki mtu kwa hila maana yake ni kumfungulia mtu kesi ya jinai bila mafanikio , na bila sababu za msingi za kufanya hivyo na mtu huyo akapata athari zozote kutokana na kumfungulia kesi hiyo. Athari ni pamoja na kupotezewa muda, gharama, usumbufu, kudhalilishwa, kupata hasara kibiashara au kikazi kutokana na kushikiliwa na kila kitu ambacho kimekuwa kama matokeo ya kusingiziwa kesi ni athari kwa maana hii.
2. SABABU ZA KUWABAMBIKIZA WATU KESI.
Sababu za kumuuzia mtu kesi huwa ni nyingi. Ni nyingi kutokana na kuwa kila aliyebambikizwa kesi huwa kuna mgogoro nyuma uliosababisha jambo hilo na migogoro kawaida inatofautiana. Pamoja na hayo sababu kuu za kubambikizia mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa au kulipiza kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro kama nilivyosema.
3. WELEDI WA ASKARI WETU NA KUWABAMBIKIZIA RAIA KESI.
Wakati mwingine askari wetu huwabambikizia watu kesi katika mazingira ya kushangaza kabisa. Askari anaweza kumbambikizia raia kesi kwasababu tu raia amehoji jambo fulani. Kwa mfano mtu anaweza kumuuliza askari nioneshe kitambulisho chako kabla hujanikamata. Utasikia askari akimwambia mtu unajifanya mjuaji tutaona, mara unanifundisha kazi utanitambua n.k. Eti mazimgira kama hayo kwa askari wetu utakuwa tayari ni mgogoro na mtu atapofikishwa kituoni basi ni rahisi kupewa kesi ambayo si yake ilimradi tu askari aoneshe kuwa aliposema utanitambua, utaona alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kweli.
Thubutu!!! sio askari wa Tanzania, hapo ndio utapata kesi million...chezea askari wa Bongo weye. Wewe mwanasheria nionyeshe kesi moja tu ya waliombambikiziwa na wakafungua kesi na kushinda.
ReplyDelete