Na Bashir Yakub.
Mara nyingi nimeandika kuhusu mirathi lakini zaidi nimegusia habari ya usimamizi wa mirathi . Leo nimeona ni muhimu kueleza mgao wa mirahi kwa kuangalia nani anapata nini kupitia Sheria ya mirathi ya serikali. Fuatana nami.
( A ) MGAO UKOJE IKIWA MUME AMEFARIKI AKAACHA MJANE, WATOTO NA NDUGU ZAKE.
Kama mume amefariki na akaacha mjane na watoto basi moja ya tatu ( 1/3) ya mali za marehemu zilizo kwenye mirathi anatakiwa apewe mke wake. Mbili ya tatu( 2/3) ya mali hizo itaenda kwa watoto wake.
( B ) MGAO UKOJE KAMA MAREHEMU HAKUACHA WATOTO LAKINI KUNA MJANE.
Kama hakuna watoto walioachwa na marehemu katika familia husika lakini kuna mjane ,mali ya marehemu hugawanywa katika mtindo ambao ndugu hupewa nusu (1/2), na mjane hupewa nusu ya mirathi ya marehemu(1/2). Hii ni sawa kwa sawa.
(C)MGAO UKOJE IWAPO MAREHEMU HAJAACHA NDUGU WALA MTOTO ISIPOKUWA MJANE TU.
Kama marehemu hajaacha ndugu wala mtoto au watoto basi mali yote huchukuliwa na mjane.Ndugu kwa maana ya hapa ni kaka, dada, mama mzazi wa marehemu au baba n.k.
( D ) KAMA MKE AMEFARIKI NA KAMUACHA MUME NA WATOTO JE MGAO UKOJE.
Hapo juu tumeona mume akifariki akamuacha mke na watoto mke huchukua moja ya tatu na watoto au mtoto mbili ya tatu. Hali iko hivohivo kwa mume naye ana haki kama alizo nazo mke wake yaani kupata mirathi kutoka katika mali za marehemu.Kwa maana hiyo mume hupata moja ya tatu(1/3) ya mali za marehemu mkewe na mbili ya tatu (2/3) huenda kwa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...