Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania  Ujerumani UTU e.V,Peter Kazaura (pichani) anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo 02.02.2015 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa Taifa. 

Akiwa nchini atafanya mazungumzo na uongozi wa taasisi mbali mbali zikiwepo  TIC, Basata, Wizara ya Ardhi,Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo pamoja na mashirika ya NSSF, NHC,  Tanzania Diaspora Initiative.

Mazungumzo hayo yatalenga upatikanaji wa Fursa zilizopo Tanzania kwa Diaspora. akiendelea kueleza msemaji wa Umoja huo wa Watanzania wanaoishi ujerumani wangependa pia kuhusishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu.

naye  Mwenyekiti wa  Umoja huo,Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kuwepo kwa safari ya Makamu Mwenyekiti,Peter Kazaura na  alisema  UTU e.V imechukua uamuzi huo  baada ya Watanzania nchini Ujerumani kukosa nafasi ya kuongea na Rais wa Tanzania  wakati wa ziara yake nchini Ujerumani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...