Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hili cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha
Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea
1: Historia yake.
2: Aliposoma na alivyosoma.
3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)
4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.
KARIBU
Masha Allah. Mwenyeez Mungu akuzidishie umri na kila jema na lenye kheri maishani mwako. Kwa kweli ni historia nzuri sana ya Mh. Balozi: Mustafa Salum Nyang'anyi. Namkumbuka enzi hizo akiwa mbunge wa wilaya ya Kondoa arround 1980's kwa kumbukumbu za utotoni zangu kama zingali sahihi. Nimependa pia the way angali bado ana kumbukumbu ya kila tukio katika mapitio yake ya maisha katika sehemu mbali mbali alizopitia, kuanzia utotoni, alikolelewa na kusomea mote na hadi alimokuwa akifanya kazi na matukio kadha wakadhalika kwa mujibu wa historia yake. In Sha Allah, tunaitegea sikio na kuisubiri kwa tashwishwi kubwa (PT 2)
ReplyDeleteShukran za dhati kwa waandaaji, waongozaji na watangazaji wa kipindi hiki cha HUYU NA YULE.