Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla ameendelea na ziara zake za kukagua maendeleo ya miradi mbali mbali ya maji,ambapo safari hii ilikuwa ni mkoani Kilimanjaro na alianzia wilaya ya Mwanga.

 Katika ziara hiyo amekutana na kuongea na uongozi wa wilaya ya Mwanga na baadae kuongozana nao katika ukaguzi wa miradi ya maji iliopo kwenye vijiji vya Kisanjini,Msangeni na Lomwe na pia alikagua maandalizi ya vifaa na eneo patakapojengwa mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe utakaogharimu dola za kimarekani milioni 41.5.

Akiongea na wananchi kijiji cha njiapanda unapojengwa mradi huo,Mh. Makalla amesema amefurahishwa na mkandarasi kuanza kazi na amewataka waanchi kutoa ushirikiano na wawe waaminifu kwa wale watakaopata ajira.Mradi huo utachukua miezi 31 na utanufaisha vijiji 17 vya wilaya ya Same, vijiji 16 vya wilaya ya Mwanga na vijiji 5 vya wilaya ya Korogwe
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akilakiwa na viongozi wa Wilaya Mwanga,wakati akiwasili.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akipata maelezo ya mradi wa maji wa Same,Mwanga mpaka Korogwe toka kwa Mhandisi Mshauri wa mradi huo,Bw. Sharif Salah.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongea na wananchi wa kijijji cha Msangeni,Wilayani Mwanga.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongea na Mhandisi Mshauri wa mradi Same-Mwanga-Korogwe,Bw. Sharif Salah.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongozana na Mhandisi Mshauri wa mradi Same-Mwanga-Korogwe,Bw. Sharif Salah pamoja na ujumbe wake wakati wa kukagua mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...