Naibu Waziri wa Maji,Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Longido mkoani Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara za kukagua miradi mbali mbali ya maji hapa nchini. 

Katika ziara yake hiyo,alikutana na viongozi wa wilaya hiyo ya Longido na kuiagiza kampuni ya Haward Humfrey iliyofanya usanifu mradi wa maji wa Kisima cha Tembo ichukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kutopewa kazi zozote za miradi ya maji nchini kwa kusanifu mradi wa maji wa thamani ya shilingi milioni 253, mradi ambao baada ya kujengwa hautoi maji.

Pia ameagiza taarifa ya tume iliyoundwa iwekwe wazi na watumishi wa halamashauri ya Longido waliohusika kusimamia mradi huu wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kusheria.

Naibu Waziri  Makalla ameweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya bilioni 1.8 katika kijiji cha Meirugoi.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akizindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya bilioni 1.8 katika kijiji cha Meirugoi.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akifurahia vazi la kimasai alilovalishwa na wenyeji wa kijiji cha Meirugoi,wilaya ya Longido.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamojna na wananchi wa wenyeji wa kijiji cha Meirugoi,wilaya ya Longido.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...