Home
Unlabelled
mhe augustino lyatonga mrema atema cheche bungeni, asema hana ukimwi na kwamba hafi mtu hapa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Aina hii ya viongozi si kwa Tanzania ya sasa jamani sasa ndio anaongea nini????wakati ni mali jamani???
ReplyDeletePole sana Mheshimiwa Mrema, binadamu hatuko sawa, wasamehe wote na upokee yote kama ni sehemu ya maisha. Mungu azidi kuimarisha afya yako na ulitumikie Taifa kwa njia ya jimbo lako.
ReplyDeleteLa! jamani maskini mzee wa watu. This is very sad kwa kweli. Pole mzee wetu na Mola atakujaalia afya.
ReplyDeleteMbatia amuonee tuu huruma huyu mzee...Akimnyang'anya Vunjo atakufa siku si zake. Amuache tuu limsaidie kumpa hela za Ubunge aweze kujitibu.
ReplyDeleteMungu amjaalie afya. Ampunguzie maumivu, na mateso ya ugonjwa.
Anasikitisha sana..
Ila watanzania wamezidi kuchonga sana kuhusu afya za watu. Hata kama ikiwa kweli alikuwa nao inahusuuu? Wewe unayemsema mwenzio unauhakika wewe ni mzima?? Unaweza kufa kabla ya huyo aliyemgonjwa.
Pole mzee Lyatonga, ila pumsika siasa msee wangu. Matatiso ya inji hii yatakutowa roho Mungu wangu
ReplyDeleteHuyu mzee anatakiwa kupumzika na kulea wajukuu, analogue wakati wake umeshapita tunahitaji viongozi wenye muuno wa digital ili nchi isonge mbele.
ReplyDeleteWeye annon wa kwanza hovyo kabisa Mzee wa watu anatetea unga wake we unaongelea muda.. Watu wamemnyanyapaa shauri ya ubunge!!! Utu uko wapi?? Pole sana Mzee wa kiraracha.. Mungu azidi kukulinda na akupe afya njema!
ReplyDeleteAmen
Mdau wa UK.
Watu inabidi tuondokane na stigma za ukimwi. Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi siku hizi wanawa outlive hata wale ambao ni wazima wa afya. Kila siku watu wanakufa kwa ajali, magonjwa ya kisukari na moyo ambayo yanaondoa watu kabla ya siku si zao, sijui kwa nini ukimwi utumike kama njia ya ku-discret uwezo mtu ama watu kwa jamii. Ndugu inabidi tubadilike. Siasa zisizoendana na utu na busara hazifai. Sababu labda iwe ni kama Mrema anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake, hii ikiwa regardless ya ugonjwa. Na kwa hili Mrema inabidi atumie busara zake kuji-assess na kuona kama kuna ukweli ndani yake. Kama upo, ni busara zaidi kuachia ngazi ili kujipa muda mzuri wa kuangalia afya yake vizuri zaidi kwani combination ya kansa na sukari inahitaji hasa mtu kupata mapumziko mazuri ili kuupa nafasi mwili kuadjust na madawa makali etc na kwa kufanya hivyo pia Mrema atakuwa ametoa nafasi kwa mtu mwingine kuendeleza pale anapoishia. Kupokezana vijiti ndio maisha.
ReplyDeletePole sana Mzee wangu Lyatonga Mrema. Ninakuombea kwa Mwenyenzi Mungu akujaalie afya njema Mzee.
ReplyDeleteninakuomba umsamehe kijana wako James. Ninajua (kama ninavyomjua James Mbatia) hawezi kutamka maneno hayo juu yako - simtetei, lakini katika hali ya kibinadamu James ni mmoja wa watu (ninaoamini) wenye hofu ya Mungu. Background yake Mzee Mrema unaielewa fika, tena bila shaka yoyote. Hakuna asiyejua sasa hivi wewe na James hamuwezi kuwa marafiki sana kwa sababu urafiki wenu umeingiliwa na ubinafsi, yaani wa kisiasa. Kila mmoja lazima auze bidhaa yake kwa kuchafua mwingine, lakini kwa situation yako ninaamini hana sababu ya kufanya hivyo (vya kukusingizia Ukimwi). Mimi si wa KV lakini ninakumbuka ulishawahi kuahidi wapiga kura wako kuwa ulikuwa ukigombea kwa mara ya mwisho (nisamehe kama nimeotea). Angalia isije ikawa ni wale akina sisi na njaa zetu wanaanza kuwachonganisha kwa sababu zao (za njaa). Njaa kali mzee watakula wapi wasipochonganisha? na hivi wanajua nyie wote mtapewa zile za Gratuity - lazima ziliwe! Msipiganie tu siasa baba, kumbuka '... no permanent enemy/friend in Politics'.
Hana jipya la kusema maana mwisho wa UBUNGE wake ni October, 2015 maana Watu wa Vunjo watamtowa mbio akiwa na Ukimwi au ikiwa hana
ReplyDelete