JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANGAZO.
MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA
NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.
Wizara ya Nishati na
Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na
kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara
inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa
kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri
zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa
Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1
Julai, 2014.
Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni
zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya
Uchimbaji Madini (Mining Development
Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi
na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na
Sheria ya Local Government Finance Act,
Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka
zilizokuwa zikilipwa awali.
Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU
KATIBU MKUU
25 Februari, 2015
Safii sana. Haya ndo mambo Serikali inatakiwa kufanya kwa wananchi wake. "Charity begins at home".Hivyo,wenyeji wa maeneo yenye raslimali ndo wanatakiwa kufaidika zaidi. It's a call that's been long awaited for!!It's about time CCM ikazinduka usingizi mnene!!Mnatuweka ktk hali ngumu sisi wafuasi wenu!!!!!KEEP UP THE GOOD WORK!!!!!!
ReplyDelete