Balozi wa promosheni ya Airtel Yatosha zaidi na msanii nyota wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu' akiwasiliana kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, katika droo iliyochezwa katika Makao Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam jana, ambapo wateja watatu wa mtandao huo, Namtapika Seif Kilumba wa Mtwara, Ramadhan Mohamed Dilunga wa Kimanzichana Pwani na Mwajabu Omari Churian wa Manzese jijini, waliibuka washindi na kutwaa gari aina ya Toyota IST kila moja. Anayeshuhudia (kushoto) ni Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Mkulima toka mkoani Pwani Ramadhani Dilunga miaka 53 na Mwalimu mstaafu wa Mtwara bw, Namtapika Kilumba (60) ni miongoni mwa Watanzania watatu walioibuka washindi kwenye droo ya kwanza ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Washindi hao kila mmoja ameibuka mshindi wa gari aina ya IST Toyota mpya, ikiwa ni siku chache tu tangu kuzindulia kwa promosheni hiyo.

Airtel Tanzania wiki iliyopita ilitangaza dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake wanaojiunga  na bando za Airtel Yatosha  gari moja kila siku kwa siku 60 ambapo mwishoni mwa wiki tayari magari matatu yalipata washindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...