DSC_0100  
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini. Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1. “Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
DSC_0239
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
DSC_0140
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...