Mwanamitindo,Tausi Likokola akiwasili leo wa uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitoke nchini Marekani kwa ziara ya siku 10 kushoto ni mama mdogo,Beatrice Likokola
Mwanamitindo,Tausi Likokola akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo Tausi Likokola akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kundi la wanne Star mara baada ya kuwasili wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda
Mwanamitindo wa Kimataifa (Mtanzania) aishiye Ughaibuni, Tausi
Likokola amesema Watanzania wanajitahidi mno katika tasnia ya mitindo, hivyo wanatakiwa kuwa na ubunifu wa
kipekee kutokana kuwepo kwa ushindani katika tasnia hiyo.
Tausi ameyasema hayo mara baada ya kuwasili
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,amesma kwa miaka
aliyoishi katika nchi za Ujerumani na Marekani, kwa sasa ndio ameona watanzania
wakionesha ubunifu wao ni mwanzo mzuri na wanaweza kufika mbali.
Tausi amesema anatarajia kufanya ushiriki wa
shughuli za kijamii, kwani ndio wajibu wake kama mwanamitindo kutokana na kuwa
mchango wake unahitajika katika jamii zenye mahitaji maalum.
Katika ujio wa Mwanamitindo huyo,Tausi anatarajia kutembelea shirika lisilo la Kiserikali
linaloshughulikia watu wanaoishi na
virusi (WAMATA) kutokana na kuwasaidia kwa kila hatua pamoja na kuzuru visiwa
vya Zanzibar.
‘’Nimekuja katika ziara yangu hii nitafanya
masuala ya kijamii lakini na uzinduzi wa mafuta ya marashi hapa nchini na
nimeona uzinduzi huu ni ufanyie nchini kwetu iwe ni fahari yangu’’amesema Tausi
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...