Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akisisitiza jambo mbele ya
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na Wahariri wa vyombo vya habari ulikuwa na lengo la kuwapa fursa pana
wahariri kuuliza maswali mbalimbali kuhusu ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akibadilishana mawazo na Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda(katikati) na Mhariri wa gazeti la Jamhuri
Manyerere Jackton.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akifurahia jambo na viongozi wa
Jukwaa la Wahariri. Neville Meena(katikati) ni Katibu na Absalom Kibanda ni
Mwenyekiti. (Picha na Abuu M. Kimario)
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju(tai nyekundu) akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu n Utawala Bora Bw. Bahame
Tom Mukiria Nyanduga wakati alipofanya ziara fupi kwenye ofisi hiyo leo jijini Dar-es-
salaam. Wengine kwenye picha ni Makamishna wa tume hiyo na Katibu Mtendaji Bi.
Mary Massay(kwanza kulia)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...