Na Sultani Kipingo
Mapango maarufu ya Amboni mkoani Tanga ni eneo kubwa kuliko yote lenye majabali ya chokaa katika Afrika Mshariki. Yapo takriban kilomita nane hivi Kaskazini mwa mji wa Tanga, njia ya kuelekea huko ikichepuka huko toka barabara kuu ya Tanga-Mombasa.
Kumbukumbu zilizopo zinaonesha mapango hayo yalizuka kiasi cha miaka milioni 150 iliyopita, katika zama za mijusi wakubwa ijulikanayo kama Jurassic age.
Eneo lake lina kilomita za mraba 234, na kwa mujibu wa watafiti, eneo hilo lilikuwa chini ya maji yapata miaka milioni 20 iliyopita.
Ndani ya eneo hilo kuna jumla ya mapango 10, ila hadi sasa ni mawili tu yatumikayo kwa watalii wa ndani na nje, watafiti na wanafunzi wa somo la jiografia wanapofanya ziara za kimasomo.
Mnamo mwaka 1892, kampuni ya Amboni iliyokuwa inalima katani mkoani Tanga, ililichukua eneo hilo, na baadaye ikaiarifu serikali ya mkoloni ya Uingereza wakati huo kuhusu mapango hayo, na mara moja ikaamuliwa mapango ya Amboni ni eneo la hifadhi tokea mwaka 1922.
Mnamo mwaka 1892, kampuni ya Amboni iliyokuwa inalima katani mkoani Tanga, ililichukua eneo hilo, na baadaye ikaiarifu serikali ya mkoloni ya Uingereza wakati huo kuhusu mapango hayo, na mara moja ikaamuliwa mapango ya Amboni ni eneo la hifadhi tokea mwaka 1922.
Haijulikani ni lini hasa mapango ya Amboni yaligunduliwa lakini ripoti zinaonesha kuwa wenyeji wa mkoa wa Tanga walikuwa wakiyatumia kama sehemu ya matambiko, jambo ambalo inasemekana hadi hii leo linaendelea.
Mnamo mwaka 1963, Serikali ya Tanganyika wakati huo, kwa kuona umuhimu wa mapango hayo kihistoria na kihifadhi, ikaamua kuyakabidhi kwa Idara ya Mambo ya Kale kwa usimamizi. Hadi leo mapango ya Amboni yapo chini ya Idara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, mapango ya Amani huvutia watalii, watafiti na wanafunzi kwa vivutio vya kusisimua, ikiwa ni pamoja na jinsi mamilioni ya popo hutoka mapangoni na kwenda kutafuta riziki nje kila jua linapotua. Wingu kubwa jeusi la popo huziba lango kuu kwa muda wakati wanyama hao wanapotoka kwenye mapango hayo ya giza.
Vile vile katika mapango hayo kuna miamba yenye maumbo kama ya sofa, meli, mamba, tembo, kichwa cha simba dume, ramani ya Afrika na hata kile kinachoonekana kama mnara wa Uhuru wa Marekani “Statue of Liberty”
Sehemu ya mapango ya Amboni mkoani Tanga
Utalii wa ndani
Bango la Idara ya Mambo ya Kale
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...