Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote bila kuvunja sheria. 
 Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji. 
“Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema Pinda 
Aliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji. 
 Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha. 
Hata hivyo Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko. 
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha. 
 Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili. 
“Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akivunja Bunge mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Mhe Christopher Ole Sendeka, akijibu hoja za wabunge kuhitimisha mjadala.Kamati hiyo iliundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Aridhi, Kilimo, Mifugo,Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe Sabrina Sungura aichangia hoja.
Mbunge wa Gando Mhe Khalifa Suleiman akichangia taarifa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...