BONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'
ametamba kumsambalatisha Fadhili Majiha 'Stopper' katika raundi za awali za mpambano wao utakaofanyika siku ya jumamosi ya feb 28 katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano huo wa raundi nane unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini ususani vitongoji vya Kinondoni, Manzese, mabibo na Mwananyamala ambapo ndio maeneo yao yenye wapenzi wao wa ngumi na sehermu mbalimbali
akizungumza na mwandishi wa habari hizi Miyeyusho ametamba kuwa atokuwa na mzaha siku hiyo itakuwa kazikazi mana yeye ni bondia mkubwa sana hapa nchini na akuna mtu wa kumbabaisha kwa sasa katika uzito wake
mbali na mpambono huo wa utangulizi kutakuwa na mpambano wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaowakutaniosha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka kutoka Morogoro ambao watatanguliwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha Shomari Mirundi zidi ya Mwinyi Mzengela wakati Shedrack Ignas atapambana na Husein Mbonde, na Godfrey Slive atamenyana na Sadick Abdulazizi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...