Ule usemi wa za mwizi ni arobani,umetimia leo baada ya vijana wawili wanaotumia pikipiki (majina yao hayakupatikana mara moja) wenye utaalamu wa hali ya juu wa kukwapua simu za mikonini za watu wawapo kwenye magari au hata watembea kwa miguu kushindwa kufurukuta mbele ya wananchi wenye hasira.
Tukio hilo limetokea jioni hii mbele ya bustani ya Botanical kwa upande unaotazamana na geti kuu la kuingia Hospitali ya Ocean Road, baada ya kumkwapulia simu mwanadada mmoja (jina kapuni) aliekuwa akitembea kwa miguu na kwa bahati nzuri kulitokea msamalia aliekuwa na gari yake akaliona tukio zima na hapo ndipo alianza kuwafukuzia na mwisho wa mbio hizo ndio ukafika hapa baada ya kuzidiwa maarifa na pikipiki yao, hali iliyowapelekea kuanguka eneo hilo.Vijana hao walikamatwa na pikipiki yao ikachomwa moto.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,akiwasimulia watu waliofika kwenye tukio hilo namna mambo yalivyokuwa mpaka kufikia kuchomwa moto kwa pikipiki hiyo yenye nambari za usajili T 636 CXX.
Taswira za kuwaka moto kwa pikipiki hiyo zikiendelea kuchukuliwa.
Mdau akijipatia Selfie mbele ya pikipiki iliyokuwa ikiteketea kwa moto wakati huo.
Hapo wamewafaidisha wenye pikipiki kwani watalipwa bima yao swaafiii#mshiko
ReplyDeletekwa nini hawajawachoma wenyewe moto!!!
ReplyDeleteSasa piki piki ndio inaiba.
Si kweli kama ambavyo mdau wa kwanza ufikiriavyo....malipo ya bima hayaendeshwi kirahisi kama udhaniavyo watakwama padogo tu.....vinginevyo labda uwe na nia ya kuwatamanisha wajitokeze ili wadakwe!!!
ReplyDelete