Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akiongozana na jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande  (watatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa kwanza kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Ally LILA  wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.
  jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuzindua wiki ya sheria nchini yanayofanyika katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake wakati akizindua wiki ya sheria nchini katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Majaji waliokaa mbele wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika wiki ya sheria nchini.

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameitaka jamii kuacha kuchukua sheria mkononi na badala yake waviache vyombo vya dola vifanye kazi yao kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni jambo la dhuluma na aibu.
 
Aliyasema hayo February 1, 2014 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fursa ya kupata haki: wajibu wa serikali,mahakama na wadau."

 "ili Mahakama kutekeleza majukumu hayo lazima wananchi wajengewe uelewa juu ya shughuli za mahakama zinavyoendeshwa na hilo ndio lengo la maadhimisho haya,"Alisema Mwinyi Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajijengea utaratibu wa kuisadia mahakama pindi panapo hitajika ushahidi ili kuepuka kuachiliwa huru kwa wahalifu wao kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Alisema kuwa sheria pia inahitaji Majaji na Mahakimu watoe haki kwa kuzingatia sheria hivyo ni wajibu wa wananchi na jamii nzima kushirikiana na  mahakama kupata haki halali kwa watuhumiwa wetu.Kwaupande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman alisema kuwa mahakama imedhamiria kutoa elimu kwa ummma kuhusu masuala mbalimbali ya kimahakama.
 
Alisema kuwa wamejipanga katika kutoa elimu kuhusu ufunguaji na uendeshaji wa mashauri  mbalimbali,utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu muafaka pamoja na mfumo mpya wa kulipa tozo za mahakama kwa njia ya benki. "kwa mara ya kwanza mahakama ya tanzania imeamua kushirikisha jamii katika kujifunza jinjsi utendaji kazi wa mahakama unavyofanya kazi ni matumaini yetu kuwa jamii itajifunza vyema na kutii sheria za nchi"alisema Chande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...