UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI
ASILIA
1.
Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata
na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji
wa gesi asilia.
2.
Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015,
EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi asilia, muundo wa mtaji (capital
structure) na faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa
mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.
3.
Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba
EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:
(a) kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na
kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;
(b) tozo kwa huduma ya kuchakata na
kusafirisha gesi asilia iwe Dola za
Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;
(c) faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane
(18%) na muundo wa mtaji wa asilimia
hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na
(d) mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa
ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa
kwa EWURA.
4.
Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha
Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014,
EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu
uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja
mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la
Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy
Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya
Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi
uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo.
5.
Tarehe 8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano
na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo
EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata
maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini,
Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC.
Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa
ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye
kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.
6.
Katika kikao chake cha tarehe 19
Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya
EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha
miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho
TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA
iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo:
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...