Idhaa ya Kiswahili ya BBC inataka kuwatahadharisha wasikilizaji na watumiaji wa mtandao wake wa bbcswahili.com dhidi ya wahalifu wanaotumia jina la BBC kuwahadaa na kutaka kuwatapeli watu.

Kumezuka mtandao bandia unaotumia jina la BBC SWAHILI NEWS kuandika habari za uzushi na kulaghai wananchi kwa habari zisizokuwa na ukweli wala uhusiano na shirika hili la habari.

BBC inapenda kuwakumbusha wasikilizaji na wasomaji wake wote wanaofuatilia habari zake kuwa makini. BBC inaufahamisha umma wa wazungumzaji wa Kiswahili kuwa haina blog ya aina hiyo na kwamba habari zote rasmi zinapatikana kupitia bbcswahili.com au bbc.co.uk/swahili na kupitia Facebook katika facebook.com/bbswahili – kinyume na hapo jihadhari sana.

Matapeli hawa wanaandika habari za uongo kuhusu watu maarufu, lakini lengo lao ni kutaka kulaghai watu watoe fedha au watoe maelezo yao binafsi ambayo yatatumiwa kwa uhalifu.

Tayari mamlaka husika zimepewa taarifa za vitendo hivyo, BBC haitahusika kwa hasara au athari itakayotokana na mtu kutapeliwa kwa njia iliyoelezwa au nyingineyo kinyume na kazi zinazofanywa na BBC.

Yoyote atakayehisi mwenendo wa aina hii atoe taarifa kupitia swahili@bbc.co.uk  au piga simu 0222 701752.

BBC Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...