TIB Development Bank, taasisi kuu ya fedha nchini katika maendeleo, pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wametia saini makubaliano ya ushirikiano (MOU) ya ufadhili wa miradi ya miundombinu kwenye Serikali za Mitaa.

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na Mh. Jumanne Sagini, Katibu Mkuu TAMISEMI na Bw. Peter Noni, Mkurugenzi Mtendaji, TIB Development Bank yanaimarisha msingi wa taasisi hizi mbili wa uboreshwaji mifumo na utoaji wa huduma bora kwa jamii na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania

Mamlaka za Serikali za Mitaa zinawajibika kikatiba kutoa na kuendesha huduma muhimu za kijamii kwa maendeleo na usawa wa kijamii. Utoaji wa huduma hizi unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu. Kuhusu hili, Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bw. Peter Noni alieleza, “TIB imebuni bidhaa mpya ya mkopo kutoa mwega wa kifedha kwa miundombinu ya Manispaa, kwa miradi inayofaa, kama vile maji, maji taka, umeme, masoko ya mazao, vituo vya mabasi na mipango miji ambayo itasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kukidhi upungufu wa fedha.” Mpango mkopo utawezesha TIB kusaidia TAMISEMI kutekeleza mpango wao wa maendeleo wa miaka mitano.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu alisema, “Makubaliano haya na TIB yamekuwa yakipikwa kwa miaka mingi. Tayari tunashirikiana kwenye miradi kadhaa, kama vile ya Soko la Kibaha, Mji Pembezoni wa Mwabepande, Kituo cha Basi cha Ng’angamfumuni na Soko la Lokolova huko Moshi. Mwega wa kifedha kutoka TIB utasaidia kuharakisha kuendeleza na kutekeleza miradi yetu ya miundombinu.

Akitambua taasisi hizi kama watangulizi katika kutekeleza mipango yetu ya maendeleo, Waziri wa Nchi Mheshimiwa Hawa Ghasia alinena, “Kwa vile bajeti ya serikali kuu na za mitaa haitatuwezesha kufanikisha malengo yetu ya muda mfupi na wa kati, ubia huu utazisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza wajibu wao wa kutoa huduma bora zitowapatia maisha bora Watanzania wote.”
Katibu Mkuu wa TAMISENI Mh. Jumanne Sagini na Bw. Peter Noni, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Development Bank wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa miradi ya maendeleo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mh. Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi, TAMISEMI, waliosimama wapili kushoto na Naibu Waziri wa Nchi, TAMISEMI.
Mh. Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi TAMISEMI akizungumza machache baada ya utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara yake na TIB Development Bank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...