Barabara ya Tunduma-Ikana-Laela hadi Sumbawanga ikiwa imekamilika kwa asilimia mia moja (100%), barabara hii ambayo ni kiungo muhimu cha Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora imejegwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Msaada kutoka kwa watu wa Marekani.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mjini Sumbawanga tarehe 02/02/2015 katika viwanja vya Nelson Mandela akiwa ziarani Mkoani Rukwa kukagua ujenzi unaoendelea wa barabara za lami za Tunduma-Ikana-Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Matai-Kasanga na Sumbawanga-Kanazi-Kizi-Kibaoni hadi Mpanda. 

Katika hotuba yake hiyo aliwaahidi wananchi wa Mkoa wa Rukwa juu ya dhamira ya dhati ya Serikali iliyopo madarakani kukamilisha ujenzi wa barabara za lami kuunganisha Mikoa ya Mbeya-Katavi-Kigoma na Tabora. Alisema hayo yatafanikiwa iwapo wananchi watatoa ridhaa kwa Serikali iliyopo madarakani kuendelea kuingoza nchi kwa miaka mingine mitano ijayo iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

Mradi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga umekamilika kwa asilimia mia moja na Mhe. Waziri ameahidi Wizara yake kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya barabara zilizobakia zikiwemo barabara za Manispaa ya Sumbwanga na zile za Wilaya ya Nkasi. Kwa ujumla fedha alizoahidi kusaidia eneo la Manispa na Wilaya ya Nkasi ni zaidi ya Tsh bilioni nne. 

Kwa mujibu wa Mhe.  Magufuli miradi yote mikubwa ya ujenzi wa barabara Mkoani Rukwa inagharimu fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni mia nane (800), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Serikali iliyopo madarakani (CCM)
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta akitoa salam za pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Msaada wa watu wa Marekani katika kusaidia ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa.  
Baadhi ya viongozi katika meza kuu wakifuatilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagwa kwa shangwe na wananchi wa Mjini Sumbawanga mara baada ya hotuba yake nzito kuhusu ujenzi wa barabara iliyowafurahisha wengi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela tarehe 02/02/2015. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza leo tarehe 03/02/2015 kwenye ziara ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli wa pili kushoto ambapo aliishukuru Wizara ya Ujenzi kwa juhudi ilizofanya katika ujenzi unaoendelea wa barabara za lami Mkoani Rukwa. Pamoja na hayo ameiomba Serikali kupitia Wizara hiyo kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiteta jambo na Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli muda mfupi kabla ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa na kuendelea na ziara yake Mkoani Katavi leo tarehe 03/02/2015. Picha  na Hamza Temba.
Kwa picha na habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...