Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi. Sabine Dall’Omo, wakati akifafanua jambo, alipomtembelea Waziri wa Uchukuzi akiwa na ujumbe wake, kutaka kufahamu fursa za uwekezaji katika sehemu ya reli, leo asubuhi.
Wakurugenzi wa Wizara ya uchukuzi, na ujumbe wa kampuni ya Siemens kutoka nchini Afrika Kusini wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi Sabine Dall’Omo( wa nne kutoka kulia), wakati Afisa huyo na Ujumbe wake walipotembelea Wizara ya Uchukuzi, kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Siemens, Bw. Kevin Pillay, akiwasilisha mada, wakati ujumbe wa Kampuni hiyo ulipomtembelea Waziri wa Uchukuzi, leo asubuhi kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...