Mkuu wa vipindi wa East Africa Radio, Nasser Kingu (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua kampeni ya Zamu yako 2015, Kulia kwake ni Mkuu wa Masoko Eatv & East Africa Radio, Alex Galinoma.
KITUO cha Televisheni chenye ushawishi mkubwa kwa vijana nchini Tanzania, EATV, sambamba na kituo chake cha East Africa Radio, mapema leo wamezindua rasmi kampeni kubwa na ya aina yake ijulikanayo kwa jina la ZAMU YAKO 2015.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa vipindi East Africa Radio, Nasser Kingu alibainisha kampeni hiyo inamalengo mahususi kwa Taifa ikiwemo vijana kwa ujumla juu ya kuwakumbusha na kuwaelimisha vijana kuhusiana na umuhimu pamoja na uwezo walionao katika kufanya maamuzi sahihi kwenye masuala makubwa ya kitaifa hususani yanayohusu siasa za Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...