Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya
Maendleo ya Jamii Bw. Xavier Keebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa
vijana kuhusu Sera ya maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Ujuzi, Mwongozo wa Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo ambapo jumla ya zaidi ya Vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa ya
Kigoma Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijini mafunzo hayo yamefanyika
katika ukumbvi wa manispaa hiyo. Kutoka Kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na
Mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo kutoka wizara hiyo Bibi. Esther Riwa.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa
akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya
Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya
Kigoma Ujiji.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga
akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya
Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya
Kigoma Ujiji.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada wakati wa warsha biliyoandaliwa na Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu Mfuko wa
maendeleo y Vijana nchini. Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma
Ujiji ambapo jumla ya zaidi ya vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa hiyo, Wilaya ya
Uvinza na Kigoma Vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...