Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa
“AirtelTunakujali” wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha
Airtel Biashara za Mashirika wameendeleza dhamira ya kusaidia jamii
kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi
iliyopo jijini Dar Es Salaam.
Airtel imeendelea kushirikiana na wafanya kazi wake kutoa mchango kwa
jamii kwa kuhakikisha shule zinakuwa na miundombinu na mazingira bora
ya kujifunza hali itakayochochea wanafunzi kupenda shule.
Uchakavu wa miundombinu ya shule hasa za msingi nchini ikiwemo vyumba
vya madarasa ni moja ya chanzo kikuu kinachodhoofisha mahudhurio ya
wanafunzi na hivyo kusababisha matokeo yasiyoridhisha.
Mwishoni mwa wiki wafanyakazi wa kitengo hicho walishiriki ukarabati
wa darasa hilo la chekechea katika shule ya msingi Ushindi lenye
kuhitaji marekebisho makubwa ambayo yanatazamiwa kuongeza hamasa ya
watoto kuhudhuria shuleni.
Akizungumza katika tukio hilo mwalimu Mkuu wa Shule ya hiyo Bw Iddi
Kaminja alisema, "tumekuwa na changamoto kubwa mahudhurio kutokana na
wanafunzi kutokufurahia kuja shuleni na hii inasababishwa na shule
kuwa na miundombinu chakavu isiyowapa ari ya kusoma.
"Tangu mpango huu wa ukarabati ulipotangazwa wanafunzi wamekuwa na
shauku kubwa ya kutaka zoezi hili liweze kuisha na kuanza kutumia
darasa hili. Hali hii limekuwa faraja kwetu hivyo ni wazi kwamba
itatusaidia kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni na hatimaye
kuongeza kiwango cha elimu hapa shuleni."Aliongeza Mwalimu Kaminja
Aidha Mwalimu Kaminja ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafanayakazi wa
Airtel kwa moyo wao wa kujitolea kwa hali na mali kuinua kiwango cha
elimu ya awali na kutoa rai kwa makampuni mengine kuona umuhimu wa
kuborosha madarasa ya shule za awali na msingi kwani njia mojawapo ya
kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ni kuwapa watoto wetu mazingira
mazuri na yenye usalama wawapo hapo shuleni.
Nae meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii Hawa Bayumi
alisema,"madarasa mazuri ni muhimu kwa usalama wa wanafunzi lakini
pia huleta hamasa ya mahudhurio hivyo ni lazima wazazi wawe tayari
kusaidia hatua za haraka kufanyia matengenezo ya mara kwa mara ili
kuepusha hatari na gharama kubwa ya fedha. Kwa njia hiyo madarasa haya
yatadumu.
"Leo tumeshiriki zoezi hili katika shule ya msingi ya Ushindi lakini
kazi hii imekuwa ikifanyika sehemu mbali mbali nchini kupitia mradi wa
“Airtel Tunakujali” ambao unawawezesha wafanyakazi wa Airtel nchi
nzima kushiriki katika shughuli za kijamii hususan zinazoinua sekta ya
elimu Tunajisikia furaha kuwekeza katika jamii kwa kiwango ambacho
kinaleta tofauti kubwa.
Siku zote tumelenga kufikisha huduma bora na
za gharama nafuu kwa watanzania huku tukitambua na kupambana na
changamoto mbalimbali za jamii inayotuzunguka.
"Leo nanyi mnashuhudia utofauti wetu na makampuni mengine, Airtel sio
tu inaongoza katika mtandao ulio bora hapa nchini bali pia namna
tunavyojali wanaotuzunguka" aliongeza Bayumi.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakiupamba ukuta kwa viganya vya mikono vilivyopakwa rangi nyekundu wakati waliposhiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es
Salaam.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni
‘B’, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni
‘B’, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakigawa zawadi kwa watoto wa chekechea baada ya kushiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...