Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini wametembelea kituo cha watoto yatima cha Huruma Children  Center kilichopo Mtaa wa Morombo  na kuwafariji pamoja na kuwapeleka zawadi.

Katika Ziara hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya jamii media ambao ni wamiliki wa  jamiiblog.co.tz  ililenga kuwakutanisha Wanahabari na makundi maalumu katika jamii ikiwa ni njia ya kujitoa kwa jamii na kuwa faraja kwa waliokosa faraja.

Mkurugenzi wa Jamii media ,Pamela Mollel amesema kuwa mbali na kuripoti matukio mbali mbali yanayojiri nchini Wanahabari wana jukumu la kuisaidia jamii kwasababu wao ni sehemu ya jamii .
Pamela Mollel ameeleza kuwa suala la kujitoa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la kila Mtanzania ili kuwasaidia kuwa na maisha bora na kuisaidia jamii pia.

Mwandishi wa Kituo cha TV 1 Mkoani hapa Jane Edward ameeleza kuguswa na watoto hao wenye vipaji lukuki ambavyo vikiendelezwa wanaweza kuwa tunu ya taifa na kuliletea taifa ushindi katika sanaa na michezo.
“Watoto hawa licha ya kuwa yatima wana uwezo mkubwa ambao ukitumiwa vizuri unaweza kulisaidia taifa letu wengine ni wabunifu mashirika binafsi ,serikali na mtu mmoja mmoja kuwaunga mkono watoto hao” Alisema Jane Edward 

Mmiliki wa blogu ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emmanuel anasema kuwa ni wakati sasa kwa wanahabari kuwa mfano wa kuigwa katika kuisaidia jamii na kuongoza mabadiliko wanayoyataka kuyaona badala ya kuwa wasemaji peke yake hususani katika masuala ya kijamii ushiriki wao utaleta mabadiliko chanya na ushawishi mkubwa.
 Waandishi wa Habari wa Arusha wakitoa Zawadi zao za "Valentine's day" kwa watoto wa kituo cha Huruma Children's Trust Kwa Morombo, Jijini Arusha, kama ishara ya Upendo na Kuwajali watoto yatima katika siku hii muhimu ya Wapendanao. Kushoto aliyesimama ni Mratibu wa Shughuli hiyo Bi. Jane Edward Kutoka TV1 -Arusha. Zawadi hizo zilitolewa Tarehe 14.02.2015 Jumamosi.
 Wakurugenzi wa Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel na Jamii Blog Bi. Pamela Mollel tukitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wa Huruma Children's Trust Centre Kwa Morombo, Jijini Arusha. kama ishara ya Upendo katika Sherehe ya siku ya wapendanao
 Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima Bw. Ferdinand Shayo na Mwandishi Huru na Mmiliki wa Blog ya Wazalendo 25 Blog Bw. Gadiola Emanuel Wakishusha mzigo ambao ni moja ya zawadi ya Upendo kwa Watoto yatima wa Kituo cha Huruma Children's Trust Centre, Kwa Morombo, Jijini Arusha. Tarehe 14/ 2/2015 Jumamosi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...