Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw. Levi Nyakundi (kushoto) akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Yatosha Zaidi bi. Mwajabu Omary leo katika makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania. Anayeshuhudia (katikati) Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano bi Beatrice Singano Mallya .Airtel imekabidhi magari matatu katika hafla hiyo.
KAMPUNI Ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo asubuhi imekabidhi magari kwa washindi watatu wa kwanza wa promoseni ya Yatosha Zaidi.
Hafla hiyo fupi ya kuvutia ilifanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Airtel na wageni waalikwa kadhaa.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi aliwaomba washindi kuendelea kutumia mtandao wa Airtel kwani kwa sasa wao ni sehemu ya familia ya kampuni hiyo.
Washindi hao ni mkazi wa mkoani Pwani, Ramadhan Dilunga (53) ambaye ni mkulima, mwalimu mstaafu na anayeishi Mtwara, Namtapika Kilumba (60) na mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam, Mwajabu Churian (27).
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mawasiliano Bi Beatrice Singa Mallya alisema: “Tukio hili la leo linaweza kuchukuliwa kama mwanzo wa mipango mingi iliyopo kwenye kampuni yetu. Kuna mambo mengi yanakuja na madhumuni yetu makubwa ni kushiriki katika kubadilisha na kuboresha maisha ya Watanzania kadhaa wenye bahati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...