Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto) akizungumza na Makatibu Kata wa CCM, Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi leo. Katika mazungumzo hayo yaliyojumuisha Makatibu Kata zaidi ya
30, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanazunguka katika kata
zao kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa
ajili ya maandalizi ya kuipigia kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Katikati
Meza Kuu ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mussa Liliyo akifuatiwa na Mwenyekiti
wa Makatibu Kata hao, Ally Napepa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani
Lindi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu wa CCM Wilaya
ya Nachingwea, Mussa Liliyo wakati alipokuwa akimwakikishia mbunge wao, kuwa timu
ya Makatibu Kata wake wamejipanga kikamilivu katika kuwahamasisha wananchi jimboni
humo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kuipiga kura Katiba
iliyopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani
Lindi, Mathias Chikawe (wanne kushoto-mstari wa mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na Makatibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimboni humo baada ya
kuwapa somo makatibu hao la kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kujitokeze kwa
wingi kujiandikisha kwa ajili ya kuipiga kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Picha zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...