Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda ameupongeza uongozi wa NMB kwa kubuni bidhaa bora na
zinazoendana na watanzania wa kada zote akitolea mfano wa akaunti za Chap Chap.
Mh Pinda aliyasema hayo alipotembelea banda la NMB katika hoteli ya St. Gasper ya mkoani Dodoma
ambapo PSPF wanafanya mkutano wao na NMB kama mdau mkubwa ameshiriki na kuweka mabanda
ya huduma mbalimbali zikiwemo za NMB Wakala, NMB E- statement na Chap Chap Instant Account
kwaajili ya washiriki wa mkutano huo.
Akaunti za Chap Chap ni za haraka na kumchukua mteja takriban dakika 10 tu kufungua akaunti na
kupata ATM card papo hapo. Tekinolojia hii ni ya kipekee na inaweza kumfanya mtu akafungua akaunti
yake popote alipo na kuanza kufaidi huduma mbalimbali kutoka NMB kupitia matawi Zaidi ya 170 na
ATM mashine Zaidi ya 600 nchini kote.
Unangoja nini kuwa na akaunti ya NMB kama huduma zimerahisishwa kiasi hicho? NMB Karibu yako
Zaidi.
Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa kitengo cha biashara ya
jumla wa NMB Ndugu Richard Makungwa juu ya huduma zaChap Chap Instant Acount na NMB Wakala.
Huduma ya NMB Wakala humuwezesha mteja kutoa na kuweka fedha kupitia mawakala wa MaxMalipo
waliotapakaa nchi nzima.
Maafisa wa NMB wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda na viongozi mbali
mbali kutoka PSPF nje ya ukumbi wa Mkutano wa St Gasper ambapo Mkutano mkuu wa Nne wa wadau
wa PSPF unafanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...