
Ujumbe wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukionyesha namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore jana.Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000 zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wan chi hiyo wamewezeshwa kumiliki nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia. Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya nyumba nchini humo jana.
Mkishatazama hayo maendeleo na mipango miji ya wengine boresheni majengo na mipango miji wilayani na mikoani, mkija mtwambie mtaanza na mikoa au wilaya gani ziwe na miundo mbinu na majengo kama Singapore siyo kwa kwenda juu ila kwa ubora wa mipango miji, maji, umememe, taa za barabarani, sewage sstem n.k. .
ReplyDeleteHii sijui ni safari ya ngapi kwa maofisa wa TZ kwenda Singapore (nafikiri na sehemu nyingine hukohuko) lakini wakirudi hapa yale yaleee, mpaka Mr Two Bungeni alishawahi kuwaita "makanjanja", kitu kama hicho!
ReplyDeleteNi mambo ya aibu!!