Na Teresia Mhagama
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress na Ujumbe wake, wamekutana
na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene, katika makao
makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao walikutana ili kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo
miradi ya umeme inayofadhiliwa na Mfuko wa Changamoto za Milenia
(MCC), mradi mkubwa wa umeme unaofadhiliwa na nchi ya Marekani
ujulikanao kama Umeme Afrika (Power Africa) pamoja na suala la
kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi
zake ili kuongeza uelewa na hivyo kuleta ufanisi wa kazi.
Waziri wa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (kulia)
akishikana mkono na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress mara
baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (kulia) akimsikiliza
kwa makini Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (wa tatu kushoto)
wakati Balozi huyo na ujumbe wake walipokutana Waziri wa Nishati na
Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Sharon Pauling, Naibu
Mkurugenzi anayeshughughulikia Ukuaji wa Uchumi katika Shirika la
Misaada la Marekani (USAID), (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi Mkaazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia nchini, Scott
Alexander.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachewene (wa pili kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (wa
tatu kushoto), wakati Balozi huyo na ujumbe wake walipokutana Waziri wa
Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Sharon
Pauling, Naibu Mkurugenzi anayeshughughulikia Ukuaji wa Uchumi katika
Shirika la Misaada la Marekani (USAID), (wa kwanza kulia), Mkurugenzi
Mkaazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia nchini, Scott Alexander (wa
kwanza kushoto) na Merrica Dominick, Afisa Uchumi na Biashara katika
Ubalozi wa Marekani nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...