Na Teresia Mhagama 
 Wizara ya Nishati na Madini imepata Tuzo ya Ki¬mataifa ya mwaka ya Maende¬leo ya Udhibiti wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi. Tuzo hiyo ya mwaka 2014 inayotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia machapisho yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY), imekabidhiwa rasmi jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ambaye alipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Wizara. 
 Tuzo hiyo, iliyotolewa na Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr inaitambua Wizara kutokana na mafan¬ikio yake katika kushughulikia changamoto za udhibiti wa sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuchochea maende¬leo ya sekta hiyo. 
 Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na sera mpya ya gesi asilia, kuwa na muundo mpya wa makubaliano ya gharama za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi (Production- Sharing Agreement), na kuwa na Rasimu ya Sera Uweze¬shaji na Ushirikishaji Wazawa (local content policy).
“Hayo ni baadhi tu ya maendeleo yaliyofanya sekta hii kueleweka na kuku¬balika zaidi kwa wawekezaji na wadau,” imesema sehemu ya Jarida la TO&GY. 
 Pamoja na Tuzo ya Wiz¬ara ya T0&GY, Shirika la Umeme nchini kupitia Mkurugenzi wake, Mhandisi Felchesmi Mramba ameshinda Tuzo ya Mtu wa Mwaka (Person of the Year, 2014) kutoka¬na na mIpango yake ya Dola za Kimarekani Bilioni Sita zitakazowezesha TANESCO kuongeza uzalishaji umeme mara tatu zaidi ya sasa kutokana na vyanzo mbalimbali kama makaa ya mawe, gesi asilia na maji hivyo kuondokana na utegemezi wa uzalishaji umeme kwa ku¬tumia mafuta. 
 Aidha Shirika la Maende¬leo ya Petroli nchini (TPDC) limeshinda Tuzo ya transition of the year (2014) kutokana na kupiga hatua katika shughuli zake ambapo mbali ya kuwa kuwa mdhibiti wa sekta ndo¬go ya mafuta na gesi bali pia limekuwa mwekezaji baada ya kushinda tenda na kupata vitalu viwili kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini. 
 Usambazaji wa machap¬isho ya TO&GY hukaguliwa na Taasisi ya Marekani ya BPA Worldwide inayokagua machapisho maalum zaidi ya 2600 katika nchi 30 Duniani yakiwemo majarida maarufu ya Toronto Star, Wall Street Journal na Gulf News.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia)  akipokea Tuzo ya Ki­mataifa ya mwaka ya Maende­leo ya Udhibiti wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi inayotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia machapisho yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY). Anayemkabidhi Tuzo hiyo ni Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr.
Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr (kushoto) akionyesha chapisho  maarufu Duniani la The Oil & Gas Year (TO&GY) linalotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani. Chapisho hilo lina habari mbalimbali kuhusu masuala ya Nishati ikiwemo fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini kupitia sekta hiyo.Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...