Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete katika picha hii ya maktaba anaonekana akimpa hongera mama ambaye amejifungua salama yeye na mtoto wake. Afya ya mama na mtoto ni moja ya ajenda ambayo inapewa umuhimu wa pekee katika duru ya Jumuiya ya Kimataifa. Tanzania na Canada kupitia wakilishi zao za Kudumu katika Umoja wa Mataifa zimeanzisha kundi la Nchi Marafiki kuhusu ajenda hiyo ya Afya ya Mama na Mtoto lengo kuu kuhakikisha kuwa mama na mtoto ni ajenda ambayo haifi.
Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Gillermo Rishechynski (pichani) mapema wiki iliyopita waliitisha kikao cha kwanza cha Nchi Marafiki kuhusu afya ya Mama na Mtoto, kikao hicho cha kwanza na ambacho kilifanyika katika uwakilishi wa Kudumu wa Canada, kilijadili pamoja na mambo mengine dhumuni la kuundwa kwa kundi hilo ambalo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto inaendelea kupewa umuhimu katika malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015, pamoja na kushawishi uwajibikaji na uwekezaji katika eneo hilo. kundi hilo linaundwa na nchi 40 kutoka mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea.
Na Mwandishi Maalum, New York
Kundi la Nchi Marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto limekutana na kufanya kikao
chake cha kwanza na kukubaliana kwa kauli moja kwamba mama anapokuwa na afya njema
anakuwa na uhakika wa maisha yake na maisha ya mtoto wake.
Kama hiyo haitoshi kundi hilo la nchi marafiki na ambalo limekutana nchi ya
uenyekiti- wenza wa Wakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Tuvako Manongi na Balozi Gillermo Rishchynski, limekubaliana haja na umuhimu wa
kuhakikisha kuwa ajenda kuhusu afya ya mama na mtoto inaendelea na kubaki kuwa moja ya
vipaumbele vya malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...