Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imeendelea kutoa msaada kwa walemavu kupitia kikundi
cha walemavu kijulikanacho kwa jina la “Tunaweza Band”, kwa
kuwawezesha kulipia gharama za kurekodi nyimbo zao mpya.
Makabidhiano
ya mkataba huo kati ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na Ontime
Production yalifanyika katika ofisi za Ontime Production iliyopo
Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’ jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Meneja wa Kitengo cha
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, amesema kuwa msaada huo ni
sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia
kuifanya kulingana na msimamo wa kampuni hiyo wa kuwa karibu na jamiii
inayowazunguka.
“Msaada huu ni sehemu ya azimio tuliloweka la kuwekeza
katika jamii yetu inayotuzunguka. Watu wanaoishi na ulemavu
husahaulika katika jamii na hawapati haki zote zinazostahili kwa
binadamu. Haki za binadamu ni sawa kwa watu wote bila kujali ulemavu
wao.
Kukosa uwezo wa kujihudumia mwenyewe, huleta mateso kwa binadamu
yeyote yule. Tunafurahi kuwasaidia wenzetu katika jamii hii kwa kuwapa
uwezo wa kujiongezea kipato kutokana na vipaji walivyonavyo.
Naye Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka alisema
kuwa amefurahishwa na moyo wa kampuni ya Airtel kwa kujali walemavu
hapa nchini kwani wao si wa kwanza kupata msaada huu kutoka Airtel.
“Nimefurahishwa sana na kitendo cha Airtel kujali walemavu hapa nchini
na kwa kutusiadia kuongeza vipaji vyetu na vile vile kutuwezesha
kuongeza kipato chetu kwani baada ya hapa tunauhakika wa kupata
mikataba ya kurekodi nyimbo zetu nyingine nyingi tu ambazo tunazo.
Kwa
niaba ya wenzangu wa kikundi cha Tunaweza, napenda kuwashukuru Airtel
kwa moyo wao wa kujali watu walio katika mazingira magumu, hasa sisi
walemavu.
Msaada huu utatuwezesha na sisi kushirIki katika shughuli
mbalimbali katika jamii pamoja na kufikia malengo yetu tuliyonayo.
Mnamo mwezi mmoja uliopita Airtel imewawezesha walemavu wengine kumi
na tano kuweza kupata mafunzo ya biashara, mtaji na vibanda vya
kisasa vya Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa
wafanyabiashara wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel
Money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel
kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es
Salaam.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akikabidhi mkataba wa udhamini kwa Meneja wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, Sixmond Mdeka, katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam , ambapo Airtel itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Wanaoshuhudia ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed (kulia) na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanamuziki wa Bendi ya Walemavu ya Tunaweza, kabla ya kukabidhi mkataba wa udhamini katika hafla iliyofanyika kwenye studio ya Ontime Production iliyopo Kijitonyama kwa Ali Maua ‘A’, jijini Dar es Salaam, ambapo Airtel
itailipia gharama za kurekodi albamu yao ya muziki. Anayeshuhudia(kulia) ni Prodyuza wa studio hiyo, Jaffari Mohamed.
Rungu mnara jamaa mwenye nyeusi....shiiiiida.
ReplyDeleteHhahahahaha jamaa mwenye nyeusi anapotezea.....
ReplyDelete