Wakaazi wa wawili wa wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kwa pamoja
wamezawadiwa magari yao aina ya Toyota IST mara baada ya kuibuka
washindi katika droo za promosheni ya Airtel yatosha Zaidi
inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Mpaka sasa jumla ya washindi 37 wameshapatikana kutoka katika mikoa
mbalimbali ikiwa bado promosheni inaendelea na magari mengi bado
yanasubiri washindi ili wakabithiwe
akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi magari kwa wateja wa Airtel
Mkoani Manyara.
Meneja wa Airtel Kanda ya Kaskazini Bwana Brighton
Majwala alisema: "Tunajisikia furaha kuendelea kupata washindi wa rika
tofauti kutoka katika maeneo mbalimbali nchini, nasikia furaha kupata
washindi kutoka katika kanda yangu.
"Hivyo naendelea kuwaasa
watumiaji wa mtandao wa Airtel na wale ambao hawajajiunga kufanya
hivyo na kupata nafasi ya kujishindia. promosheni bado inaendelea na
magari bado yapo kinachotakiwa kufanya ni kununua na kujiunga na
kifurushi chako cha Airtel yatosha zaidi na kupata nafasi ya
kujishindia.
nawapongeza sana washindi wetu wa leo na washindi wote ambao
wameshapatikana mpaka sasa.
"Na nachoweza kusema ni kwamba Airtel
tunajivunia kuwa sehemu ya kubadili maisha ya watanzania wengi hasa
walio na kipato cha chini na kuwawezesha kufikia ndoto zao huku
tukiendelea kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kupita
huduma zetu na promosheni kama hizi. ni matumaini yetu kwa kupitia
promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi watanzania wengi wataguswa na
kuboreshewa maisha yao".
Kwa upande wake Bwana Mohamed Ahmad Khamis ambaye ni mshindi wa gari
aina ya Toyota IST alisema "Nimesikia furaha kubwa sana leo kupata
ushindi huu mkubwa, kwangu hii imekuwa kama ndoto, mimi ni mtumiaji
mzuri sana wa huduma za Airtel na ninazo line tatu za Airtel na hii
moja leo imenipa ushindi. kwakweli nimeamini kabisa Airtel yatosha
zaidi na inabadilisha maisha ya watanzania.
"Nimekuwa na ndoto za
kumiliki gari lakini leo Airtel imeniwezesha kufikia malengo yangu na
kunipa ushindi huu mkubwa na kuniwezesha kumiliki gari langu,
nawashauri watanzania hasa wale wasioamini kuhusu promosheni hizi sasa
waamini na kujua kwamba ni kweli promosheni hii na ni ya uhakika kwani
mimi nimeshinda bila kuwa na taarifa yeyote. nawashukuru sana Airtel
yatosha zaidi".
Naye mama Emiliana Tarmo Hhaway ambaye alizidiwa na furaha hadi
kushindwa kuongea kwa lugha ya kiswahili alisema: "Nnamshukuru Mungu
sana kwa kuniwezesha kushinda gari hili lakini pia nawashukuru sana
Airtel kwa kuniwezesah kushinda. mimi nimenunua kifurushi cha Airtel
yatosha cha shilingi mia tano na leo namiliki gari la mamilioni ya
pesa ni jambo la kustaajabu sana. gari hili sasa litaniwezesha katika
shughuli zangu za kilimo, kutoa mazao shambani kwenda sokoni,
litanisaidia katika shughuli zangu za kijamii, kusaidia majirani hasa
tukiwa na wagonjwa na nyingine nyingi. nasema asante sana kwa Airtel
na kwa ushindi huu
Droo ya wiki ya 7 ya promosheni ya Airtel Yatosha inategemea kufanyika
siku ya Alhamisi jioni ambapo washindi wengine 7 wa wiki hii
watapatikana na kutangazwa
Staff Sergeant wa wilaya ya Hanang Janet Mungolya akimkabithi funguo mshindi wa gari aina ya Toyota IST Bwn Mohamed Ahmed Khamisi mara baada kuibuka mshindi wa droo ya wiki ya nne ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. Bi Emiliana ni mfanya biashara ndogo ndogo na mkazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara akishuhudia ni meneja mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini bwana Brighton Majwala
Staff Sergeant wa wilaya ya Hanang Janet Mungolya akimkabithi funguo mshindi wa gari aina ya Toyota IST Bi Emiliana Tarmo HHaway mara baada kuibuka mshindi wa droo ya wiki ya tano ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. Bi Emiliana ni mkulima na mkazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara akishuhudia ni meneja mauzo kanda ya kaskazini bwana Brighton Majwala
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi bwana Mohamed Ahmed Khamisi akiwasha gari lake mara baada ya kukabithiwa gari yake katika halfa iliyofanyika katika uwanja wa mnada wa edasak wilaya ya Hanang mkoani Manyara
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bi Emiliana Tarmo HHaway akifungua gari yake mara baada ya kukabidhiwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa mnada wa edasak wilaya ya Hanang mkoani Manyara
Burudani katika hafla hiyo iliyofanyika katika uwanja wa mnada wa edasak wilaya ya Hanang mkoani Manyara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...