Kamanda Mpinga na kikosi chake cha Usalama Barabarani kweli wana kazi. Ankal kalishuhudia hili wakati akirejea kutoka Dodoma kikazi kurudi Dar es salaam ambapo wakati akisafiri barabara ya Morogoro alikutana na mambo ya kutisha yanayoelekea kuendelea katika barabara zetu na kupelekea ajali za kila siku.
Kwanza Ankal alishuhudia ajali za barabarani takriban tatu hivi katika siku moja tu ya Machi 20, 2015 ambapo alishuhudia lori la semi-trela za gari (zote) za Scania ambapo ya kwanza ilikuwa kukuta lori moja likiwa limeacha njia na kupinduka karubu na kijiji cha Mdaula.
Mbele kidogo, huku mvua ikinyesha kwa nguvu, Ankal na wenzie katika gari dogo walilokuwa wakisafiria wakajikuta uso-kwa-uso na mauti, pale lori semi-trela (la Scania) lililokuwa likitokea Dar es salaam likiacha msururu wa magari mengine na kulenga njia ya magari yajayo.
Hakika zilikuwa ni sekunde kama 10 hivi za kuogoya wakati lori hilo lililokuwa linataka kupita takriban magari saba, manne kati yake yakiwa ni ma semi-trela kama hilo, likijaribu kupita foleni hiyo kwa kasi.
Dereva wa gari alilokuwemo Ankal alipiga honi, kisha akawasha ta azote, lakini bado semi-trela hilo liliendelea kuja.
Kiasi cha mita sita mbele yao ndipo dereva wa lori hilo akaweza kusimama, kwa mbinde na kuponea kugogana uso-kwa-uso na gari dogo la kina Ankal.
Kamanda Mpinga na kikosi chake wana kazi kweli. Ni dhahiri kwamba dereva wa lori hilo aidha hana utaalamu wa kuendesha gari barabarani, ama alikuwa amelewa. Ukichanganya na mvua kubwa iliyokuwa unanyesha, usalama ulikuwa haupo kabisa barabarani.
Nini kifanyike? Swali zuri sana hilo. Sensa ama ukaguzi wa leseni za madereva wote nchi nzima ufanyike haraka iwezekanavyo. Na kama ikigundulika dereva ana leseni bila kupitia mafunzo katika Chuo cha Usafirishaji ama VETA awekwe kando.
Kubwa lazima kuanzia sasa hatua zichukuliwe, na zionekane kuchukuliwa, kila inapotokea jambo kama hili ama ajali kabisa.
Lori semi-trela likikaribia kugongana uso-kwa-uso na gari dogo alilokuwemo Ankal na wenzie baada ya lori hilo kuingia sehemu ya barabara isiyo yake...na kama si ustadi wa dereva wa kina Ankal, saa hizi hii habari ingekuwa ingine hapa...
Uso-kwa-uso na lori
Mbele kidogo kuna lori liloloacha njia bila shaka kwa tukio kama ambalo Ankal alikutana nalo huko nyuma
Anko acha utani bwana , mbona huku toa namba ya gari ? Au unamuonea huruma huyo dereva Kwasababu alisimama ? Kamana Mpinga unafikiri ataanzia wapi ? Ila nakupa pole sana kwa tukio lililo kukuta !
ReplyDeleteAnkal acha woga bhanaaah!!!
ReplyDeleteMadereva wa Tanzania acheni sifa hasa wa malori munapokuwa munaendesha magari. Sifa zilimuua mbwelu, ninyi si wakwanza kuendesha magari, kwa hivyo kuweni makini. Acheni sifa na muogopeni Mungu. Acheni kuvuta bhangi munapoendesha barabarani. Tumechoka kila siku ajali, wanaosababisha ajali ni nyinyi milori ninyi. Sifa zilimuua mbwelu, naomba ujumbe huu uwafikie huko muliko. Acheni sifa barabarani.
ReplyDeleteThe mdudu, poleni sn wajomba wote kwa huo mkasa....nilikua na mpango wa kurudi ili nimpe mikakati na ubunifu ndugu yangu afande sele ili aigeuze moro mjini iwe nusu London.....coz nna uhakika atashinda kwakishindo cha ajabu 2015. .bora niongee nae kwenye phone tu kulikoni kurudi kumbe maisha bado roho mkononi....mm nahisi nchi yetu ya Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani isio fuata sheria za bara barani...na hiyo moro road ifanyeni iwe na njia 4 kupeleka 4 kuludisha...na kumbuka msemo wa babu yangu mzee mfomi (rip) aliposema mjukuu wangu kusoma sio kuelimika unaweza kusoma sn lakini ukawa mbumbumbu wa fikra na ubunifu...angalizo kwa wadau wote huu msemo ni kweli kabisa....la mwisho kabisa lawama zangu ziende kwa mjomba michuzi na wenzako siku nyingine mtu kama huyo mfikisheni wenyewe police msicheke na watoa roho za watu. ..haya mkae sarama wote huko na mpendane.
ReplyDeleteKumbe wewe mpori pori haya mkae (SARAMA )halafu tushakuchoka na comments baba bongo usirudi tuachie wenyewe mara afande sele mara ntaongea nae kwa phone nenda facebook uandike utakavyo huku tumekuchoka bwana mdudu
DeleteHapa naona ulikuwa unatafuta kisingizio tu cha kutokurudi nyumbani. Huna nia ya kweli ya kutaka kurudi nyumbani.
DeleteLa! hii ni hatari vibaya sana. Tunamshukuru Mola kukuepushia janga hili Ankal. Barabara na ziwe double lane jamani. Ujenzi uanze kidogo-kidogo tu na in 10 years barabara zote zitakuwa double lane na kupunguza vifo vingi kiasi hiki. There are more cars today and roads are still as narrow as they were in the sixties.
ReplyDeletePole kaka,sidhani kama sawala la kuover take linataka utaalamu linaitaji common sense ,nadhani pombe imechangia ,sababu pombe kwa dereva mnywaji ina kufanya uwe na over confidence .
ReplyDeleteMungu apishie mbali ajali hizi ambazo zimeathiri jamii nyingi na kukatisha maisha ya watu.
ReplyDeleteMdau wa pili toka juu ningefurahi tungekuwa pamoja maana angalau na woga wangu niliweza kulenga kamera na kufotoa...Ila kwa kweli hali haikuwa nzuri kabisa, mvua inanyesha na jamaa anakuja resi upande wetu, na hakuna pa kukimbilia maana kushoto korongo kubwa na kulia ni foleni ya magazri na mbele Scania. hadi sasa sielewi alikuwa anawaza nini dereva yule, nakubaliana na mdau kwamba huo ulikuwa ni ulevi wa viroba
ReplyDeletePole sana Ankal.
ReplyDeleteMara nyengine tujitahidi kukumbuka kuchukuwa namba za magari, alau huyo mwenye gari atambue dereva aliyemuajiri anafanya vituko gani barabarani.
Labda hwenda itasaidia kidogo.
Ankal umetustua sana lakini tumshukuru Mwenyezi Mungu. Sijui hali hii ambayo imechukua maisha ya wengi tutaikabili vipi kama Taifa. Pole sana. Nimejisikia naliona hilo lori likinijia! Shukran na poleni nyote.
ReplyDeletePole sana ankal, suluhisho ni 1. Sheria za barabarani zirekebishwe ziwe kali zenye kuhusu vifungo bila faini kwa makosa ya kizembe- zisijali kuwa huyu aliyefanya kosa ni andrew chenge au nani.
ReplyDelete2. Magari mabovu yasiruhusiwe kutembea katika barabara zetu kabisa, kuwe na utaratibu wa kukagua na kuweka stickers kutoka motor vehicle department (kama haipo ianzishwe na kuendeshwa na serikali)
3. Adhabu za faini ziondolewe kwani ni ndogo sana, uwepo uwezo wa kutaifisha na kupiga mnada magari yanayofanya makosa makubwa yanayosababisha hasara kwa barabara.
4. Kuwe na system ya kuweka rekodi kwa madereva wote wanaofanya au waliofanya makosa ya barabarani na mfumo wa kupata pointi kwa kila kosa itakayoweza kuwanyang'anya leseni madereva wazembe wanaokimbiza magari, wasababishao ajali, wasiofuata taratibu kama vile kupita taa nyekundu, kushusha abiria kusipotakiwa, kukatisha ruti, kudanganya umri na mengineyo (bila kujali huyu ni mtoto wa raisi, waziri au mkurugenzi)
5. Kwenye kutoa leseni kuwe na upimaji wa macho kutoka kwa madaktari wanaoeleweka, na pia afya. Kwa watakaofeli afya wanyimwe leseni, kwani kupewa kwao leseni kutasababisha vifo vya barabarani.
6. Adhabu ya kuendesha ukiwa umelewa iwe kunyimwa kabisa leseni.
7. Barabara kuu (mnaziita highways...wakati siyo) kama Mtwara-Dar-Arusha-Namanga. Barabara ya Dar-Tunduma-Songea; Dar-Dodoma -Mwanza -Bukoba na nyingine zenye kupitisha magari mengi zipanuliwe anagalau ziwe lanes mbili kwenda na kurudi na service lanes, hiyo pia itasaidia kuinua uchumi wa nchi yetu kwa kurahisha uchukuzi na usafirishaji kuliko ilivyo hivi sasa ambapo lori moja tu likipinduka popote iwe darajani Wami au kwingine inazuia magari ya pande zote. Tunao uwezo kabisa wa kupanua hizo barabara.
BILA HAYO KUMALIZA AJALI HIZO NI NDOTO, POLISI PIA WAFUNZWE KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HIARI BILA SHURUTI, NA IKIFAHAMIKA HATA KWA KUHISIWA YUPO ANAYEPOKEA RUSHWA AFUKUZWE MARA MOJA NA APELEKWE MAHAKAMANI.
Hizo ndoto tu ndugu yangu... km upo majuu. Ukweli ni kwamba. Yoote usemayo viongozi wanayajua. Wanaenda nchi zenye maendeleo kiila cku. Wanatibiwa huko hawayataki kuyaleta maendeleo nyumbani. Wao wanayafuata hukohuko. Barabara na rushwa kila kona vitabakia ivyo ivyo.
DeleteNakubaliana na wewe asilimia mia. Madera wetu wengi hawajui udereva. Udereva sio kuendesha gari pekee, ni pamoja na kufata sheria za barabara. Ni kweli lane moja haitoshi zinahitajika zaidi ya lane mbili. Ajali Zinatokea sababu watu wanaover take kwa kubahatisha bila kuwa na uhakika kama kuna gari inakuja opposite side. Zikiongezwa lanes za barabara, na elimu kwa madereva wote especially defensive driving na kuongeza viwango vya fines ikiwepo jail time. Itasaidia. Nchi zilizoendelea wapo madereva wakorofi, lakini Wanafata taaratibu sababu fine ni kubwa na adhabu zingine ikiwepo jail na kuwapo record. Inayomnyima mtuhumiwa hata kupata ajira sehemu nyingine.
DeleteAnnon wa kwanza, niliyoyaandika ninaona ni suluhisho, tunahitaji nguvu kuyasimamia.....kama ni bungeni au kuishinikiza serikali na hao viongozi wake wasio wasikivu kwa sababu haya mambo ya ajali yanawaumiza watanzania wote haijalishi vipato vyetu. Tuwe na mapendekezo mengi ili hata kama haitawezekana kuyafuata yote angalau yale machache yatakayofuatwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa, mfano tuseme kuna hayo mapendekezo saba, tukifuata mawili amabayo ni kupanua barabara zetu kuu na kudhibiti mwendo kasi.....kwa kiasi kikubwa itapunguza ajali sana, tunahitaji kuwa na ushirikiano na mawazo chanya kuwa tunaweza na tutaweza hata kama itakuwa ni suala la kampeni. TUPIGE KELELE, Tutaweza kukomesha ajali.
DeletePoleni sana mlionusurika !!Hiv nilinitutapata kiongozi katili kidogo,siasa aweke kando, iwekwe sheria ya kuwaadhibu wazembe papopapo, viboko vya tumboni hadharani mara ufanyapo kosa. nafikiri maumivu yake sijui kama atarudia tena,..adhabu nyingine zote watu wamekuwa sugu.
ReplyDeleteANKAL, PROPOSAL YAKO YA VETA SIIAFIKI, UTAKUTA HUYO JAMAA AMEATEND VETA NA CHUO CHA USAFIRISHAJI NA AME_QUALIFY. TO ME THE MOST CHA MUHIMU NI HAWA JAMAA BARABARANI KUACHA RUSHWA, NAKUWAADHIBU MADEREVA KWA MAKOSA YAO. PAMOJA NA KUWEKA TIME REGISTRY AND CONTROL POINTS. KWA MFANO, UKIINGIA SERENGETI NA KUTOKEA GETI LINGINE WANAANGALIA MUDA ULIOINGIA NA KUTOKA, KAMA UMEOVERSPEED MAANA YAKE UTATUMIA MUDA MCHACHE KULIKO UNAOTAKIWA, THEN UNAPIGWA FAINI.... VIVO HIVYO WALITAKIWA WAWE NA TIME REGISTRY POINTS AMBAPO ATA_REGISTER NA KUWA CHECKED KWENYE SECOND POINT,
ReplyDeleteMARA NYINGI HAWA MADEREVA WANA USHINDANI WA KIJINGA, KITENDO HICHO ALICHOFANYA HUYU DEREVA KIKIRIPOTIWA NA VITHIBITISHO KAMA VYAKWAKO, ANATAKIWA AADHIBIWE HASWA.
MTU MWENYE BUSARA HAWEZI KUOVERTAKE MAGARI SABA KWA MARA MOJA, LAZIMA KUNA INFLUENCING FACTOR, (i.e bangi pombe na madawa mengine...) hivyo kuwe na physcal test za hizi influencing factors kwenye sehemu nyingi. aidha kuwe na tabia ya kuwapa madereva semina elekezi mara kwa mara
Hari ya nchi imeasha-change, Tanzania inatakiwa kupanua Barabara zake. 2-kwenda 2-kurudi. na zianze na zile zinanzo ingizia serekali kiwango kikubwa cha uchumi wake.
ReplyDelete2.na ninakubaliana na mtoa maoni hapo juu. Udereva sio kuendesha gari pekee, pia ni kufuata sheri za barabarani.