Mhe.Liberatus Mulamula
Balozi wa Muungano ya Jamhuri ya Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatus Mulamula, alipozungumza katika kongamano la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani, aliwataka wanaDiaspora wa nchi za kiAfrika kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na watalaamu wa vitengo vya afya duniani ili kuboresha upatikana wa huduma za afya barani Afrika. Mhe. Balozi Mulamula, ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alizungumzia faida za kutumia Teknolojia ili kuboresha mawasiliano kati ya wataalam, utafiti na elimu .
Nia mojawapo ya kongamano la Global Health Catalyst Cancer Summit 2015 ni kuboresha huduma mahiri za saratani barani Afrika kwa kutumia ( Information and Communication Technologies (ICTs);Teknolojia ya mawasiliano kati ya wataalam wa gojwa la saratani wa nchi za nchi za ng'ambo na wataalam waliopo barani Afrika.
Mhe. Balozi L. Mulamula, alikabidhi Tunzo Maalum kwa Bigwa wa Tiba ya Saraatani Dr. Twalibu Ngoma. Dr.Ngoma ni miongoni mwa wataalam wa kuigwa ambaye amepata elimu ya juu nje ya nchi na kureja nyumbani ili kuboresha upatikanaji wa huduma na elimu ya saratani nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...