Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa
mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya
kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace
Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na
kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye
ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati),
ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga. akiongea wakati wa tukio la
kumuaga na kumkabithi bendera ya taifa kwa ajili ya
kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace
Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na
kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye
ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. pichani katikati ni
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA), Nsao Shalua akifatiwa na mshindi wa Airtel Trace Music
Stars, Mayunga Nalimi.
mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika
bendera mara baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na
Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya muziki ya
Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika Jumamosi hii nchini Kenya.
Barasa la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindano
la Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi
kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha
washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku
ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.
Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa
vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music
lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi
na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini
ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa
februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na
katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million
50.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...