Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo.
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na benki hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...