Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mororogoro leo imetengua adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka na badala yake atatumikia kifungo cha nje na kulipa fidia ya Shilingi milioni moja.
Cheka alikuwa akikabiliwa na kosa la kumpiga na kumjeruhi Bahati Kibanda, ambaye alikuwa ni meneja wa baa yake iitwayo Vijana Social Hall iliopo mjini Morogoro.
Cheka anatumikia kifungo chake cha nje kwa kufanya kazi za serikali kwa muda wa masaa manne kila siku kwa kipindi chote cha kifungo hicho.
Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka akipatiwa maelekezo kutoka kwa askari.Picha na Maktaba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...