Mwanasoka wa kike, Melanie Gines (kushoto) ambaye ni raia wa Hispania na  bondia Omari Kimweri na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa tayari kupanda ndege na kurudi kwao 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto)  akimkabidhi glove kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati ni  bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchiniAustralia. Omari Kimweri ambaye aliongozana nchini na mwanasoka huyo muda mfupi kabla awajapanda ndege kurudi kwao.
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi nchini Australia amempiga tafu ya vifaa vya kufundishia kocha wa kimataifa wa mchechezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 
wakati wa zihara yake ya wiki mbili ya kutembelea nyumbani kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu zitumiwazo na mabondia wa nje
kabla ya hapo bondia huyo aliongea na wadau mbalimbali wa masumbwi wakati wa mchezo wa ngumi za kulipwa kati ya Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumbo mpambano uliofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kumvalisha mkata wa ubingwa bondia wa uzito wa juu Mchumiatumbo baada ya kuibuka na ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza
siku hiyo pia alimpiga tafu kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kwa kumkabidhi vifaa vipya vya kufundishia mchezo wa masumbwiakizungumza baada ya kumkabidhi vifaa kocha Super D alisema amekumbuka nyumbani kwa kuwa ndio alipo zaliwa na kitovu chake kimezikiwa hapa nchini hivyo ataendelea kuwakumbuka zaidi kwa kuwawezesha mabondia kucheza mara kwa mara pindi atakapoanzisha Kimweri Promotioon itakayoshilikiana na Super D Boxing Coach And Promotion kwa kushilikiana kuwapatia mabondia kupigana ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea kipato pamoja na kupandishe rekodi zao kwa mabondia chipukizi
nae kocha Super D alishukulu kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ambavyo vitamsaidia kuendelea kuinua mabondia mbalimbali chipkizi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...