Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

Chuo Kikuu cha Uhio nchini Marekani kinaendesha mafunzo kwa vijana ya kuwa viongozi bora katika nchi zilizopo katika jangwa la Sahara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Katibu wa Kwanza wa Mawasiliano ya Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini,Marissa Maurer amesema kuwa program ya kutoa mafunzo kwa viongozi vijana imaeazishwa na Chuo Kikuu Cha Uhio nchini Marekani  ambapo fedha inayoendesha mafunzo ni ya serikali ya watu Marekani (USAID).

Marissa amesema vijana wanafursa hivyo kwa mafunzo wanayoyapata yatawajenga kuwa viongozi bora wa kuhudumia jamii zao.

Alisema Program hiyo inajulikana kama Yalli Camp imeanzishwa mwaka 2010, baada ya mzunguko wote wa mafunzo kwa vijana watafanya tathimini kuona kama vijana wamekuwa na mabadiliko kupitia mafunzo hayo.

Kwa upande wa Vijana ambao wanapata mafunzo hayo akiwemo Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassary amesema mafunzo hayo yamekuja katika muda mwafaka kutokana na uhitaji uliopo wa vijana.

Joshua alisema vijana wa sasa hawawezi kujitoa na vijana katika nchi mbalimbali kutokana na dunia kuwa kama kijiji hivyo ni lazima vijana wawe sehemu ya mabadiliko.
Alisema miaka ya nyuma vijana walipewa nafasi wakavurunda hali ambayo vijana walionekana sio waaminifu hivtyo kwa sasa vijana tutumikie.
Mkurungenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya waandishi wa habari,na Pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha OHIO,kilichopo Marekani,Dkt. Yusuf Kalyango,akitoa Mafunzo kwa vijana ya kuwa viongozi bora katika nchi zilizopo katika jangwa la Sahara,mafunzo hayo yaliandaliwa na serikali ya marekani.
Muwezesaji wa Mafunzo kwa vijana ya kuwa viongozi bora katika nchi zilizopo katika jangwa la Sahara,Kofi Essien akitoa mafunzo kwa vijana hao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...