Na Yusuph Kilewo
Nilipata kuzungumzia mchango mkubwa unaopatikana kupitia vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na Tasnia ya filamu katika kutoa elimu ihusuyo maswala ya usalama mitandao. Hollywood wamekua wakiongoza katika kutengeneza vipengele mbali mbali vyenye kutoa ufafanuzi wa makosa mtandao yanavyo tendwa na namna ya kutambua na kujikinga.
Hatua yao hiyo imekua ikipongezwa sana na wataalam wa maswala ya mitandao duniani kote huku tukisistiza mataifa mengine yaweze kuiga juhudi hizo. Kuungana na wataalam wengine nilipata kuandika Makala ya kingereza inayosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”, Makala iliyofanya vizuri na baadae kupatikana katika gazeti moja la ughaibuni linalotoka maramoja kila mwezi.
Mwezi huu wa tatu Hollywood wameamua kuzindua tamthilia maalaum iliyopewa jina la CSI: CYBER ambapo imejikita katika maswala ya usalama mitandao. Katika tamthilia hiyo inatoa mafunzo mbali mbali kwa kuonyesha makosa yanavyo fanywa na namna ya upelelezi wa makosa hayo unavyo fanyika pia.
Mwandaaji wa Filamu Hiyo Amekiri kua kilicho mvutia kuifanya si tu hamasa kutoka kwa wataalam wa usalama mitandao bali pia ni pamoja na uhalisia kua kila siku ni lazima habari za uhalifu mitandao zitengeneze vichwa vya habari huku akiamini wengi wata tamani sana kuona filamu ihusuyo mambo wanayosikia sasa katika vyombo mbali mbali vya habari yahusuyo uhalifu mtandao. Kupata chanzo na kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...